Makubaliano ya Huduma ya Kutengeneza na Kuposti Posters
1. Utangulizi
Tanclick Company Limited inatoa huduma ya kutengeneza posters za kibiashara kwa ajili ya wateja wanaotaka kuimarisha muonekano wa biashara zao mtandaoni.
2. Maelezo ya Huduma
Mteja atatengenezewa posters 20 kwa mwezi.
Posters zitatumwa kila siku ya kazi (Jumanne hadi Ijumaa), moja kwa siku, hadi kukamilisha jumla ya posters 20 kwa mwezi.
Huduma hii inagharimu Tsh 20,000 kwa mwezi, malipo yakifanyika mwishoni mwa mwezi husika.
3. Huduma ya Ziada (Optional)
Endapo mteja atakuwa na majukumu mengi au hatopata nafasi ya kuposti, Tanclick itamsaidia kuposti matangazo yake moja kwa moja kwenye ukurasa wa Instagram wa biashara yake.
Huduma hii ya kuposti itatozwa Tsh 20,000 kwa mwezi.
4. Gharama za Jumla
Huduma ya kutengeneza posters pekee: Tsh 20,000 kwa mwezi.
Huduma ya kutengeneza + kuposti posters: Tsh 40,000 kwa mwezi.
5. Masharti
Malipo hufanyika mwisho wa mwezi baada ya huduma kukamilika.
Mteja atawasilisha taarifa muhimu (kama vile bidhaa, bei, na maelezo ya matangazo) kwa wakati ili kurahisisha utengenezaji wa posters.
Poster zitatengenezwa kwa ubunifu wa kipekee na haziwezi kurekebishwa zaidi ya mara moja bila makubaliano mapya.
6. Hitimisho
Kwa kujiunga na huduma hii, mteja anakubali masharti yaliyotajwa hapo juu. Tanclick Company Limited itahakikisha utoaji wa huduma kwa ubora na kwa wakati, ili kuimarisha muonekano wa biashara yako mtandaoni.